Vacancy Details
POST:
AFISA MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA II - (LIVESTOCK FIELD OFFICER II) - 5 POST
EMPLOYER:
MDAs & LGAs
APPLICATION TIMELINE::
2025-02-19 2025-02-28
JOB SUMMARY:
NIL
DUTIES AND RESPONSIBILITIES:
i.Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake;
ii.Kufanya kazi pamoja na Wakaguzi wa afya ya wanyama, kukagua nyama na usafi wa machinjio;
iii.Kukusanya takwimu za nyama na mazao yatokanayo namifugo kama ngozi na kuandika taarifa;
iv.Kutibu na kutoa chanjo za magonjwa ya mifugo chini ya usimamizi wa daktari wa Mifugo na kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa;
v.Kutembelea wafugaji mara kwa mara na kuwapa ushauri wa kitaalam katika eneo lake la kazi;
vi.Kukusanya takwimu zote za maendeleo na magonjwa ya mifugo katika eneo lake la kazi na kutoa taarifa;
vii.Kushauri na kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio na miundombinu inayohusiana na ufugaji bora;
viii.Kusimamia uchanganyaji wa dawa ya josho;
ix.Kusaidia katika uhamilishaji (Artificial Insemination) na uzalishaji (breeding) wa mifugo kwa ujumla;
x.Kushauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa, nyama, mayai na utunzaji wa mifugo; na
xi.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na fani yake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE:
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma- NTA Level 6) ya mojawapo ya fani ya Uzalishaji Mifugo; Uzalishaji Maziwa na Kuku; Afya ya Mifugo na Uzalishaji; Ukaguzi wa Nyama kutoka Vyuo vya Wakala wa Mafunzo ya Mifugo au sifa inayolingana na hiyo kutoka chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
REMUNERATION:
TGS.C